PIERRE-EMERICK Aubameyang amewaambia rafiki zake kuwa anataka kuhamia Manchester United badala ya Arsenal. Hiyo ni kwa mujibu wa gazeti la Starla Uingereza.
Mshambuliaji huyo wa kimataifa wa Gabon, yupo kwenye orodha ya wakali wanaotakiwa na United kiangazi hiki na klabu hiyo ina matumaini ya kumpeleka Old Trafford kwa kusaini dili la pauni milioni 60.
Aubameyang mwenye umri wa miaka 26 anayekipiga katika klabu ya Borussia Dortmund inayoshiriki Bundesliga, pia amekuwa akimezewa mate na Arsenal kwa muda mrefu, lakini anatarajiwa kuwaacha 'solemba' na kuchagua kwenda United.
Hata hivyo, United haina kazi rahisi kumpata Aubameyang kwani inatarajiwa kukumbana na ushindani mkubwa kutoka baadhi ya klabu kubwa za Ulaya, ikiwamo Real Madrid ambayo nyota huyo aliwahi kusema kuwa angelipenda kuichezea siku moja.
Comments
Post a Comment