MTAALAMU aliyebobea katika masuala ya soka, Alvise Cagnazzo amefichua kuwa Manchester United ipo kwenye mazungumzo na Juventus juu ya usajili wa mshambuliaji raia wa Argentina, Paulo Dybala mwenye thamani ya zaidi ya pauni milioni 50.
United ambayo inahaha kusuka upya kikosi chake kwa ajili ya msimu ujao bila kujali itakuwa na kocha gani, imekuwa ikihusishwa na uhamisho wa mshambuliaji huyo wa zamani wa Palermo katika wiki za karibuni.
Dybala mwenye umri wa miaka 22, aliyechagua kujiunga na Juventus badala ya Arsenal kiangazi kilichopita, amepiga mabao 16 katika mechi 34 alizocheza katika msimu wake wa kwanza akiwa na 'Kibibi Kizee' cha Turin.
]
Cagnazzo amelidokeza gazeti la Sun kwamba anaamini kuwa Rais wa Juve, Andrea Agnelli, ataruhusu mshambuliaji huyo kuuzwa kwa bei inayofaa na kudai kuwa tayari mazungumzo yameanza kati ya United na miamba hiyo ya Serie A.
Comments
Post a Comment