Kwasasa hivi club nyingi zinatamani kuwa na mchezaji mdogo na mwenye kasi na uwezo wa kufunga kama Paul Dyabala. Lakini kabla ya kujiunga na Juventus, AC Milan na Inter Milan walijaribu kwa karibu sana kumpata mchezaji huyu.
Kesho watacheza mechi dhidi ya Inter Milan club ambayo ilitaka kumsajili kabla ya Juventus. Dyabala amesema, "Kabla sijaja Juventus kocha wa Inter Milan Roberto Mancini alinipigia simu mwenye na kuniambia nia yake ya kutaka kuwa na mimi Inter Milan. Lakini siku zote nilitaka kujiunga na club ambayo inashinda makombe ambayo ni Juventus"
Akizungumzia mechi ya kesho dhidi ya Inter Milan amesema,"Ni mechi kubwa kwenye ligi ya Serie A na tutafanya kadri tunavyoweza kupata ushindi huo muhimu kama tunavyojaribu kufanya kwenye kila mchezo ambao tunacheza"
Kuhusu mechi yao ya marudiano dhidi ya Bayern amesema,"Tutaenda kucheza hiyo mechi Jumatano, itakua mechi ngumu lakini itabidi tupigane hadi mwisho.Kila kitu kinawezekana angalia Liverpool walichofanya dhidi ya AC Milan na kushinda Champions League, inabidi tucheze dakika 90."
Mechi ya Juventus Vs Inter Milan itaonekeana Live kwenye Startimes channel ya World Football kesho Jumapili saa 4:00 usiku.
Cheki skills za Paulo Dybala
Comments
Post a Comment