NI MCHUANO MKALI DIEGO SIMEONE NA ANTONIO CONTE UKOCHA WA CHELSEA



NI MCHUANO MKALI DIEGO SIMEONE NA ANTONIO CONTE UKOCHA WA CHELSEA
Italy manager Antonio            Conte is expected to become the Chelsea boss next season
ROMAN ABRAMOVICH ameripotiwa kukutana na Kocha wa Atletico Madrid, Diego Simeone akiwa katika harakati zake za kuamua kocha ajaye Chelsea, wakati Mtaliano Antonio Conte anayeinoa timu ya taifa ya Italia – Azzurri akisubiri kutangazwa.

Bilionea huyo raia wa Russia anayemiliki klabu hiyo, amekuwa katika mawindo ya kocha mpya Stamford Bridge kufuatia kutupiwa virago kwa Jose Mourinho Desemba mwaka jana, ambaye pengo lake limezibwa kwa muda na Guus Hiddink.

Simeone na Conte wote wamo kwenye orodha ya makocha wanaowindwa na Abramovich, lakini ripoti zinadai kuwa Conte ndiye aliye kwenye nafasi nzuri ya kupewa kibarua, akitarajiwa kutangazwa hivi karibuni kutokana na wawakilishi wake kutua London na kufanya mazungumzo.

Lakini kwa mujibu wa Gazzeta World, Abramovich alisafiri kwenda Uholanzi ambako alikutana na Simeone na kufanya naye mazungumzo, hali inayoonyesha kuwa bilionea huyo bado anapima wa kumtwisha mzigo.


Comments