MANCHESTER UNITED KUMSAJILI WINGA FEDERICO BERNARDESCHI WA FIORENTINA


MANCHESTER UNITED KUMSAJILI WINGA FEDERICO BERNARDESCHI WA FIORENTINA

MANCHESTER United wameripotiwa kumtolea macho winga Federico Bernardeschi wa Fiorentina na mipango inafanywa kuhakikisha wanamaliza biashara mapema, ili waweze kumtumia msimu ujao.

Winga huyo wa kimataifa wa Italia anayecheza katika kikosi cha nchi hiyo cha vijana wa chini ya miaka 21, amekuwa miongoni mwa wachezaji wanaong'ara msimu huu, ambapo tayari amepachika mabao matano katika mechi 22 akiwa na kikosi cha Paulo Sousa.

Bernardeschi mwenye umri wa miaka 22, aliyefunga bao dhidi ya Tottenham katika Europa League Alhamisi iliyopita, amejifunga kuichezea Fiorentina hadi mwaka 2019.


Hata hivyo, kwa mujibu wa gazeti la Sun, United inayojiandaa kwa mara nyingine kumwaga fedha nyingi kusuka kikosi italazimika kwanza kuzipiku Real Madrid na Paris Saint-Germain kuweza kupata saini ya winga huyo anayethaminishwa kwa pauni milioni 20.


Comments