MANCHESTER CITY NI KAMA VILE IMESHATINGA ROBO FAINALI YA CHAMPIONS LEAGUE ...PSV Eindhoven yabanwa na Atletico Madrid nyumbani
Machester City ikicheza ugenini, imeibuka na ushindi mnono wa 3-1 dhidi ya Dynamo Kiev na kunusa hatua ya robo fainali ya Ligi ya Mabingwa barani Ulaya.
Katika mchezo huo wa hatua ya 16 bora, magoli ya City yalifungwa na Sergio Aguero dakika ya 15, David Silva dakika ya 40 na Yaya Toure (dak ya 90) wakati bao pekee la Dynamo Kiev liliwekwa wavuni na Vitaly Buyalsky katika dakika ya 59.
Katika mchezo mwingine wa hatua hiyo ya 16 bora, PSV Eindhoven ilishindwa kutumia vema uwanja wa nyumbani kwa kulazimishwa sare ya 0 - 0 na Atletico Madrid.
Comments
Post a Comment