Wakati Memphis Depay akihangaika kufunga kwa mipira ya adhabu ndogo kwenye kikosi cha Manchester United, Juan Mata amefunga goli ambalo kwa macho ya kawaida linaonekana ni goli rahisi sana.
Depay alitua United akiwa na sifa nyingi za kuwa mtaalamu wa kupiga mipira iliyokufa lakini hadi sasa bado hajaonesha utaamu huo. Mata alifunga bao hilo dhidi ya Shresbury Town na kuisaidia timu yake kusonga mbele kwenye michuano ya FA Cup kwa ushindi wa bao 3-0.
Smalling alianza kuifungia United bao la kuongoza dakika ya 37 kisha Mata kupiga bao la pili dakika ya 45 kabla ya Lingard kukamilisha ushindi wa bao 3-0 ka bao lake la dakika ya 61.
Manchester United imefuzu kucheza hatua ya robo fainali ya FA Cup ambapo itakutana na West Ham ikiwa kwenye uwanja wake wa nyumbani Old Trafford.
Angalia video ya magoli yote matatu ya Manchester United vs Shresbury Town.
Comments
Post a Comment