TIMU ya Manchester City inasemekana kuwa na mpango wa kumtafutia mkataba wa miaka kumi katika kampuni ya Adidas kiungo wanayemuwinda katika timu ya Juventus, Paul Pogba.
Kwa mujibu wa jarida la Gazzetta dello Sport, mkataba huo na kampuni hiyo ya nchini Ujerumani, utakuwa na thamani ya pauni mil 31. Kiasi ambacho kitamfanya mfaransa huyo kuwa miongoni mwa wachezaji wenye fedha nyingi.
Hata hivyo mchezaji huyo wa timu ya taifa ya Ufaransa anasemekana kujikuta kwenye vita kubwa baada ya kampuni ya Nike nayo kuonyesha nia ya kumtaka, lakini inavyosemekana ameshakubaliana na kuhusu mkataba huo wa mamilioni ya pauni.
Wakala wa mchezaji, Mino Raiola, alisema juzi kuwa ndio yupo katikati mwa mazungumzo baina ya pande hizo mbili na akasema kuwa Pogba anatarajiwa kuwa sura ya Adidas ACE 16+ purecontrol.
Kwa sasa tetesi zinazidi kushika kasi zikielezea kuwa Pogba atajiunga na Manchester City wakati timu hiyo itakapokuwa chini ya kocha Pep Guardiola kuanzia majira haya ya joto.
Comments
Post a Comment