LIVERPOOL YAJIPANGA KUMSAINISHA KIUNGO IGNACIO CAMACHO


LIVERPOOL YAJIPANGA KUMSAINISHA KIUNGO IGNACIO CAMACHO

LIVERPOOL inajipanga kuanza mazungumzo kuhusu dili la kumsainisha kiungo mkabaji wa Malaga, Ignacio Camacho.

Staa huyo wa zamani wa Real Madrid alikuwa akifuatiliwa kwa karibu na wasaka vipaji wa Liverpool miezi iliyopita na kuvutiwa naye na sasa mtandao wa Bleacher unaripoti kuwa klabu hiyo inajiandaa kuanzisha mazungumzo ya kumuhamishia Anfield mwisho wa msimu huu.

Kwa mujibu wa Bleacher, imedaiwa kuwa Liver inaweza kufika dau la pauni milioni 7, ingawa Malaga kutokana na kuwa na tama ya fedha inaweza kukubali hata chini ya kiwango hicho.

Camacho mwenye umri wa miaka 25 n I mchezaji mwenye nguvu na juhudi katika nafasi yake ya kiungo cha ulinzi ambapo ana uwezo wa kudhibiti mchezo kwa pasi zake zilizokwenda shule na hodari wa kuingilia mchezo mpira unapokuwa kwa timu pinzani.


Comments