LICHA YA UMRI KUMTUPA MKONO, MICHAEL CARRICK AITOA UDENDA ARSENAL



LICHA YA UMRI KUMTUPA MKONO, MICHAEL CARRICK AITOA UDENDA ARSENAL

ARSENAL ipo tayari kujaribu karata yake kutekeleza dili la kushtua kwa kiungo wa Manchester United, Michael Carrick katika usajili ujao wa majira ya kiangazi.

Carrick, ambaye amedumu Old Trafford kwa zaidi ya miaka 10, ni mara ya nne sasa anahusishwa na Arsenal iliyofeli mara tatu majaribio yake ya kumpeleka Emirates.

Gazeti la Daily Mirror linaripoti kuwa Arsenal imeamua kujaribu tena bahati yake kutokana na ukweli kwamba kiungo huyo mkabaji mwenye umri wa miaka 34 atakuwa mchezaji huru baada ya mkataba wake kufikia ukomo kiangazi hiki.

Daily Mirror limeripoti kuwa Arsene Wenger anataka kutimiza ndoto yake kiangazi hiki bila kujali umri mkubwa wa staa huyo ambaye pia anatolewa macho na Newcastle.


Comments