Kwanini Shaffih Dauda Anasema Abdi Banda wa Simba Alistahili Kadi Nyekundu?



Kwanini Shaffih Dauda Anasema Abdi Banda wa Simba Alistahili Kadi Nyekundu?
Jumamosi February 20, 2016 umechezwa mchezo wa ligi kuu ya Vodacom Tanzania bara kati ya Yanga vs Simba (Dar es Salaam derby) na kuishuhudia Yanga ikipata ushindi wa pilli wa goli 2-0 dhidi ya Simba kwa mara ya pili kwenye msimu huu.

Mengi yamezungumzwa baada ya mchezo huo lakini huu ni mtazamo wangu baada ya kuufatilia mchezo ho kwa umakini mkubwa .

Kabla ya Abdi Banda kuoneshwa kadi nyekundu na kuiacha Simba ikiwa pungufu kwa mchezaji mmoja hali ya mchezo ilikuwaje?

Kabla ya kadi nyekundu kutolewa kwa Abdi Banda, game ilikuwa ime-balance na Simba walikuwa wameitawala Yanga kwenye eneo la midfield lakini baada ya kadi nyekundu ya Banda, ikailazimu Simba kumshusha Majabvi kwenye nafasi ya ulinzi wa kati. Katika eneo la kiungo wakabaki Ndemla, Kazimoto na Mkude Yanga wakawa wengi kwenye eneo la katikati.

Kadi nyekundu iliwaathiri kwa kiasi gani wachezaji wa Simba?

Namna ambavyo wachezaji wa Simba walivyochukulia tukio la kutolewa kwa Abdi Banda iliwashusha morali. Wachezaji wakaona tayari wapo pungufu kwenye mechi kubwa dhidi ya Yanga halafu kadi imetoka mapema ikawavunja ari. Lakini kama wachezaji wangeandaliwa kisaikolojia kabla ya mechi kwamba wanaenda kwenye mechi kubwa, tukio la kadi nyekundu linaweza kutokea wakati wowote, tukio kama hilo likitokea wanachezaje ingeweza kuwasaidia.

Je Banda alistahili kadi nyekundu?

Kadi ya kwanza ya njano aliyooneshwa Banda ukiangalia unaweza kudhani alikuwa ni mtu wa mwisho na kujiuliza kwanini hakupewa straight red card. Kwasababu watu wengi wanavyoelewa ni kwamba ukicheza rafu ukiwa mtu wa mwisho unapata red card. Lakini haiko hivyo, kadi ya njano alistahili. Na nimsifu mwamuzi kwa maamuzi aliyofanya kwa kadi ya kwanza. Kwasababu hata kama Ngoma angefanikiwa kumpita Banda tayari kulikuwa na Juuko ambaye angeweza kuokoa mpira kutoka kwa Ngoma. Kadi ya njano ya kwanza ilikuwa sahihi kabisa.

Kadi ya njano ya pili Banda alistaili bila kujalisha alishapewa kadi ya njano awali. Kwasababu sheria inasemaje? Kama alifanya makosa inabidi aadhibiwe kulingana na makosa yake bila kujali kama tayari anakadi au hana.

Nini kilitakiwa kifanyike baada ya kadi nyekundu ya Banda?

Nilifikiri kocha na benchi lake la ufundi watafanya mabadiliko ya mapema kwa kumtoa striker mmoja na kumuingiza beki moja au kiungo lakini kwenye benchi lao hakukuwa na beki. Lakini ili kuweza kumudu ushindani kwenye eneo la katikati wangemtoa Kiiza au Ajib. Lakini kwa mtazamo wangu wangemchomoa Kiiza halafu waongeze kiungo kwa ajili ya kuongeza ushindani kwenye eneo la katikati.

Wakati huo wanamuongezea majukumu Ajib ya kukimbia na kupambana kwenye eneo la mbele kwasababu aina ya uchezaji wa Ajib angemudu kucheza akiwa mshambuliaji pekee.

Bila shaka yoyote kadi nyekundu aliyopewa Banda mapema iliwaathiri Simba kwa kiasi kikubwa kwa dakika zilizokuwa zimesalia kwenye mchezo.

Angalia video hapa chini uone namna Shaffih Dauda na Ally Mayay 'Tembele' walivyo dadavua kuhusu kadi nyekundu aliyooneshwa Abdi Banda.

Comments