KUELEKEA ARSENAL VS BARCELONA: UNAJUA LUIS ENRIQUE AMEWAHI KUIPIGA ARSENAL BAO 2 KWA MGUU WAKE? (Video)


KUELEKEA ARSENAL VS BARCELONA: UNAJUA LUIS ENRIQUE AMEWAHI KUIPIGA ARSENAL BAO 2 KWA MGUU WAKE? (Video)

Enrique-Barca

Kuelekea mchezo wa UEFA Champions League kati ya Arsenal dhidi ya Barcelona, shaffihdauda.co.tz inakukumbusha kwamba, kocha wa sasa wa miamba ya Catalan Luis Enrique alikuwa sehemu ya kikosi cha Barcelona kilichochapwa na Arsenal bao 4-2 kwenye uwanja wa Wembley October 1999.

Katika mchezo huo ambao Barca ililala mbele ya The Gunners, Luis Enrique aliifungia bao la pili timu yake. Wakati huo kocha wa sasa wa Manchester United Louis van Gaal pamoja na Ronald Koeman walikuwa kwenye benchi la ufundi la Barcelona.

Kwenye mchezo uliopigwa Now Camp mwaka huohuo (1999) Arsenal ililazimisha sare ya kufungana bao 1-1. Katika mchezo huo Enrique alimzunguka mkongwe wa The Gunners Patrick Vieira na kuifungia Barcelona goli la kuongoza.

Katika maisha ya soka ya kocha huyo ambaye amepata mafanikio makubwa akiwa kama kocha wa Barca, ameifunga Arsenal magoli mawili enzi hizo alipokuwa mchezaji wa timu hiyo. Unaweza kuyashuhudia magoli yake kupitia video hapa chini.



Comments