JUVENTUS            imenusurika kulala nyumbani baada ya kutanguliwa 2-0 na Bayer            Munich lakini ikachomoa na kuambulia sare ya 2-2 kwenye mchezo            wa Champions League hatua ya 16 bora.
        Miamba hiyo ya            Italia iliyocheza fainali dhidi ya Barcelona msimu uliopita,            ilikwenda mapumziko ikiwa nyuma kwa bao moja lililofungwa na            Thomas Muller dakika ya 43.
        Dakika ya 55            Arjen Robben akaiandikia Bayern Munich bao la pili na matokeo            yakabaki hivyo hadi dakika ya 63 pale Paulo Dyabala            alipoifungia Juventus goli la kwanza.
        Dakika ya 76 Stefano Sturaro akaingia            kwenye box na kumzidi maarifa Joshua Kimmich kabla ya            kumchambua kipa Manuel Neuer na kuisawazishia Juventus.
                  JUVENTUS                XI: Buffon; Lichtsteiner, Bonucci, Barzagli,            Evra; Cuadrado, Khedira (Sturaro 69), Marchisio (Hernanes 46),            Pogba; Dybala (Morata 75), Mandzukic
        BAYERN MUNICH XI: Neuer;            Lahm, Kimmich, Alaba, Bernat (Benatia 74); Robben, Muller,            Vidal, Thiago, Costa (Ribery 84); Lewandowski.
        Thomas Muller            akishangilia baada ya kuifungia Bayern Munich bao la kwanza            muda mfupi kabla ya mapumziko
        Arjen Robben anaiandikia            Bayer Munich bao la pili
        Paulo Dybala              anashangilia baada ya kuipatia Juventus bao la kwanza
        Stefano Sturaro              anamzidi maarifa Joshua Kimmich na kuifungia Juventus bao la              kusawazisha
          
Comments
Post a Comment