Juve vs Bayern: Guardiola na Jaribio la kuondoka na Heshima ya kushinda Champions League


Juve vs Bayern: Guardiola na Jaribio la kuondoka na Heshima ya kushinda Champions League

Pep Guardiola ana mtihani mzito wa kuendelea kuipa uhai ndoto yake ya kumaliza utawala wake na Bayern Munich kwa kushinda ubingwa wa ulaya.
Leo Jumanne, Bayern wamesafiri mpaka Turin kuumana na washindi wa pili wa michuano hii msimu uliopita Juventus katika mechi ya kwanza ya raundi ya 16 bora.

  Ugumu wa mechi hii ambao tayari ulishafahamika baada ya mechi hii kupangwa December, hivi sasa umezidi kwenye kipindi cha miaka hii miwili. Miezi michache baada ya kufungwa mechi tu ya fainali ya Champions League na Barca ambayo iliwazuia kutwaa 'treble'. Juventus wamekuwa na mwanzo m'baya zaidi katika Serie A. Wakiwa wameondokewa na wachezaji muhimu kama Andrea Pirlo, Carlos Tevez na, Arturo Vidal ambaye amejiunga na Bayern – ilikuwa wazi kwamba 'The Bianconeri' wangepita kwenye kipindi cha mapito.  
Kipindi hiki cha mpito kimekuwa cha haraka, timu sasa inaongozwa na vijana wa kizazi kipya ambao walikuja kuchukua nafasi walioondoka baada ya msimu uliopita, mmoja wa vijana hao wapyani – Paulo Dybala, Juventus walienda kushinda mechi 15 mfululizo kwenye Serie A na kufanikiwa kurudi usukani mwa ligi. Pamoja na rekodi hiyo kufikia mwisho kwa sare ya 0-0 dhidi ya Bologna jumamosi iliyopita, kikosi cha Massimiliano Allegri kinapewa nafasi kubwa ya kutwaa ubingwa wa 5 mfululizo wa Scudetto.

Wakati huo huo, mambo hayajaenda vizuri sana kwa upande wa Bayern. Misimu miwili ya kwanza ya Guardiola Bayern Munich iliishia kushinda ubingwa wa Bundesliga mara mbili lakini wakaishia kupata matokeo ya yasiyoridhisha katika Champions League – hasa kutokana na majeruhi ya wachezaji muhimu mwishoni mwa msimu.

  
Safari hii tofauti na misimu iliyopita – sio majeruhi tena upande wa ushambuliaji bali ni safu ya ulinzi. Jerome Boateng, Javi Martínez na Holger Badstuber hawatocheza kabisa, wakati Mehdi Benatia, anaweza kurejea na kuanzia kwenye benchi kwa sababu hajaitumikia timu hiyo kwa miezi miwili.

Majeruhi ni kitu cha mwisho ambacho Guardiola angetaka akiwa anataka kumaliza muda wake na Bavaria kwa mafanikio. Tangu droo ilipopangwa ndani ya wakati huo pia imethibitishwa Mkatalunya huyo ataondoka Bayern Munich mwishoni mwa msimu na kwenda kujiunga na Manchester City.
Kukiongoza vizuri kikosi cha wachezaji ambao wanajua kiongozi wao amechagua kwenda sehemu nyingine ni changamoto kubw. Na Guardiola anataka kuacha legacy nzuri kwa Wajerumani. Mpaka sasa Bayern wapo juu kwa pointi 8 na kwa namna inavyoenda ipo wazi Bayern watashinda ubingwa wa 3 mfululizo wa Bundesliga chini ya uongozi wake. Lakini bado hafanikiwa kupata kile wengi wanachotamani. Wikiendi iliyopita mashabiki walibeba bango pale Allianz Arena lilosomeka "Pep was never our thing anyway," – Wakimaanisha Pep hakuwa wa kwetu – jambo ambalo limeongeza mgawanyiko.

  Kwa mashabiki wengi wa Bayern bado hawajaridhishwa na Pep – Guardiola siku zote amekuwa akiandamwa mzimu ukweli kwamba alichukua Bayern ambayo ilitoka kushinda makombe yote chini ya Jupp Heynckes. Chochote isipokuwa ubingwa wa Champions League itakuwa ni kufeli kwa Pep pamoja na timu yake kufanya vizuri sana katika style ya uchezaji ya timu.

Lakini mchezo dhidi ya Juventus unaweza kuipa Bayern uhai mpya kuelekea kupata mafanikio ya Heynckes na kuondoka kwa heshima. Mara ya mwisho walipokutana mnamo mwaka 2012 – msimu ambao Bayern Munich walishinda ubingwa wa ulaya – Bayern waliwafunga 2-0 nyumbani na ugenini.

Pamoja na matatizo yote ya safu ya ulinzi – kuna hali ya kutia moyo kwa Guardiola, silaha zake za safu ya ushambuliaji zote zipo sawa – Ribery amerudi wikiendi iliyopita katika mechi ya ushindi 3-1 dhidi ya Darmstadt. Mechi ambayo ilihusisha magoli mawili mazuri kutoka kwa Thomas Muller na Robert Lewandoski – magoli hayo yamewafanya washambuliaji hao kufikisha magoli 56 katika mashindano yote msimu huu. 

  But  Kuwasili kwa Lewandowski mwaka 2014 kulipelekea kuondoka kwa Mario Mandzukic na sasa Mandzukic amehamia Juventus akitokea Atlético Madrid, Mcroatia huyo atataka kuonyesha wanachokimisi Guardiola na timu yake watakapokutana baadae kidogo.

Habari za Timu
Juventus: Allegri atakuwa bila beki wake Martín Cáceres na wachezaji wake wa upande wa kushoto Alex Sandro na Kwadwo Asamoah.
Bayern Munich: Boateng, Martínez na Badstuber watakuwa nje, usajili wa January kutoka Spartak Moscow Serdar Tasci anaweza kucheza, na tayari alishaanza kucheza wikiendi iliyopita.



Comments