BEKI wa Arsenal, Gabriel Paulista (pichani            kushoto) amesema kuwa wana mipango ya siri itakayowasaidia            usiku wa leo kuwadhibiti wauaji watatu wa Barcelona - Lionel            Messi, Luis Suarez na Neymar ambao kwa pamoja wamepiga mabao            91 msimu huu, lakini akasisitiza kwamba itabaki kuwa siri hadi            hapo mechi itakapoanza.
        The Gunners hawapewi nafasi kubwa ya            kushinda pamoja na kuwa nyumbani Emirates leo, lakini wanajua            kwamba wanahitaji kupata matokeo muhimu katika mechi hii ya            awali ya Champions League hatua ya 16 bora kama wanataka kuwa            na nafasi ya kusonga robo fainali.
        Gabriel  ambaye            hatarajiwi kucheza leo kutokana na kuwa majerehi alisema:            "Najua fomula ya kuwazuia Messi, Neymar na Suarez lakini            imefungwa kwa kufuli saba! Siwezi kuitangaza fomula. Kama            nitaitangaza, nitakuwa nahatarisha mikakati yote ya timu            iliyofanyiwa kazi. Lakini haitakuwa rahisi kuwazuia."
        Beki huyo aliongeza kuwa wachezaji wote            wanataka kuandika Historia Arsenal, kwamba wanataka kushinda            Champions League na pia Premier League.
        
Comments
Post a Comment