Bundesliga inabaki kuwa ligi ambayo inapewa support kubwa sana na mashabiki kuliko ligi yoyote ile kwa ujumla. Uwanja wa Allianz Arena mara kadhaa umekua unaingiza watazamaji 75,000 na Schalke nao wanakaribia kwa kupata watazamaji 62,271. Lakini pia Borussia nao pia wanapata wastani wa watazamaji 81,086 kutokana na mechi 10 za kwanza kwenye michezo yao ya nyumbani.
Wiki hii Bundesliga wametangaza wastani mpya na umekua namba mbili kwenye historia ya ligi hiyo. Kwa michezo yote ya mzunguko wa kwanza wa Bundesliga wamepata wastani wa watazamaji 42,344 ambapo mwaka jana ilikua ni wastani wa 42,155.
Jumla ya mashabiki ambao wameangalia michezo 153 kwenye mzunguko wa kwanza wa Bundesliga wamefikia idadi ya 6,478,680. Mashabiki wengine wanaendelea kuangalia michezo ya Bundesliga kwenye TV zao. Kuwa mmoja kati ya watu hawa kwa kuangalia Live Bundesliga kwenye kinga'amuzi cha Startimes.
Comments
Post a Comment