Jose Mourinho atakuwa kocha mpya wa Manchester United msimu ujao akimrithi Louis van Gaal, rafiki wa kocha huyo wa Kireno amethibitisha hilo.
Mkurugenzi wa Inter Milan, Bedy Moratti ambaye ni dada wa rais wa zamani wa klabu hiyo, Massimo Moratti amefichua habari hizo baada ya kupata mlo wa mchana na Mourinho siku ya Jumamosi katika jiji la Milan.
Alipoulizwa kama Mourinho atarejea Inter Milan, akajibu: " Hapana, yuko na furaha sasa, anakwenda Manchester United.
Jose Mourinho ndani ya Inter Milan
Kocha wa zamani wa Chelsea kwa sasa yuko huru baada ya kutimuliwa Stamford Bridge mwezi Disemba
Mourinho akiachia watu wajipigie 'selfie' ndani ya San Siro Jumamosi wakati alipoenda kuishuhudia timu yake ya zamani ikimenyana na Sampdoria
Mkurugenzi wa Inter Milan Bedy Moratti amefichua kuwa Jose Mourinho anakwenda Manchester United
Comments
Post a Comment