"BIASHARA imeisha". Ndivyo ilivyothibitisha klabu ya Lazio ya Italia kwamba Manchester United imekubali dili la kumsajili kiungo mshambuliaji wake Felipe Anderson kwa dau la pauni milioni 46.8.
Anderson mwenye umri wa miaka 22, alihusishwa kwa kiasi kikubwa na uhamisho kwenda United katika dirisha la usajili wa mwezi Januari, ambapo timu hiyo ilisema kuwa ilipeleka mara mbili maombi ya kutaka huduma yake.
Mipango hiyo hata hivyo iliharabika baada ya Lazio kugoma kumuuza, lakini sasa miamba hiyo ya Italia imesema tayari imemalizana biashara na United.
"Felipe Anderson atahamia Manchester United msimu ujao kwa euro milioni 60," alisema Rais wa Lazio, Claudio Lotito akiwaambia waandishi wa habari baada ya kuhudhuria mechi ya Serie B wikiendi iliyopita.
Comments
Post a Comment