STAA wa zamanai wa Manchester United, David Beckham amesema kuwa ana matumaini kocha wa zamani wa Chelsea, Jose Mourinho hivi karibuni atakabidhiwa kibarua cha kuinoa timu mojawapo ya Ligi Kuu England.
Mourinho yupo nje ya kazi tangu alipofukuzwa na Chelsea Desemba mwaka jana, lakini amekuwa akihusishwa na klabu ya zamani ya Beckham, Manchester United ambayo inasuasua ikiwa chini ya kocha Louis Van Gaal.
Kutokana na hali hiyo, nahodha huyo wa timu ya taifa ya England amesema kwamba angefurahi kuona Mreno huyo akirejea katika soka la England mapema iwezekanavyo.
"Nina matumaini Mourihno atarejea kwenye michuano ya Ligi Kuu England hivi karibuni," Beckham aliuambia mtandao wa TalkSPORT. "Tunataka makocha wenye uwezo kama huo katika soka letu."
Comments
Post a Comment