PEP Guardiola anakwenda Manchester City kuchukua nafasi ya Manuel Pellegrini, lakini kwa mujibu wa gazeti la Daily Star, kocha huyo amepigwa marufuku kuondoka na staa yeyote katika timu yake ya sasa ya Bayern Munich.
Daily Star limesema kuwa kocha huyo raia wa Hispania anayetarajiwa kuanza kibarua chake kipya msimu ujao, amepigwa marufuku hiyo kwa mdomo na maofisa wa Bayern.
Guardiola ni shabiki mkubwa wa Robert Lewandowski na ripoti zilisema kuwa amekuwa na nia ya kuambatana naye Etihad ili kuunda pacha ya safu ya ushambuliaji na Sergio Aguero, lakini kutokana na marufuku hiyo sasa atalazimika kuangalia upande mwingine.
Comments
Post a Comment