Baada ya kutangulia kwa magoli 2 dhidi ya wapinzani wao Juventus, Bavarian walijikuta wakirudishiwa magoli yote mawili na kupoteza nafasi ya ushindi muhimu nje ya nyumbani kwao.
Leo wanaingia tena uwanjani kwenye harakati za kuendelea kutetea taji la ubingwa wa ligi ya Bundesliga dhidi ya Wolfsburg. Licha ya kuwa pazuri kwenye msimamo wa ligi, kocha Pep bado anasema kila mechi ni muhimu, "Ni wiki muhimu sana kwetu, tunaweza kupiga hatua kubwa mbele baada ya hii mechi"
Msimamo wa ligi ya Bundeslifga unaongozwa na Bayern Munich ambao wana points 59 na wanaofuatia Borussia Dortmund wana points 51. Kama Wolfsburg wakiiifunga Bayern, basi Borussia wanakua kwenye nafasi nzuri kuendelea kwenye harakati za kuutafuta ubingwa.VfL Wolfsburg wapo nafasi ya 8 na points 31.
Hii ni moja ya mechi kati ya Bayern Vs Wolfsburg ambapo ya leo utaiona #Live kupitia king'amuzi cha Startimes.
Comments
Post a Comment