ARSENAL imepata hasara ya kuutumia vibaya uwanja wake wa nyumbani kwa kukubali kichapo cha bao 2-0 kutoka kwa Barcelona katika mchezo mkali wa Champions League.
Vijana wa Arsene Wenger sasa watakuwa na mlima mrefu wa kupanda Nou Camp ambapo ili watinge robo fainali, watahitaji ushindi wa 3-0.
Lionel Messi alikuwa mwiba kwa Arsenal kwa kufunga mabao yote mawili, la kwanza likija dakika ya 71 na la pili likiwasili kwa njia ya penalti kunako dakika ya 83.
Hii ni mara ya kwanza kwa Lionel Messi kumtungua kipa Petr Cech na ni mara ya kwanza kufunga ugenini dhidi ya timu za England.
Kimahesabu safari ya Arsenal kwa mara nyingine tena inakomea hatua ya 16 bora kwa mwaka wa sita mfululizo.
Katika miaka mitano iliyopita, Arsenal ilijikuta ikipoteza mchezo wa kwanza hatua ya 16 bora kwa zaidi ya goli moja. Ilipoteza 4-0 kwa AC Milan, 3-1 na 2-0 kwa Bayern Munich kabla ya kufungwa 3-1 na Monaco.
Arsenal (4-2-3-1): Cech 7, Bellerin 6.5, Mertesacker 5.5, Koscielny 6, Monreal 7, Coquelin 7 (Flamini, 81, 4), Ramsey 7.5, Oxlade-Chamberlain 5.5 (Walcott, 50, 6), Ozil 6, Sanchez 7 Giroud 5.5 (Welbeck, 73, 6.5)
Barcelona (4-3-3): Ter Stegen 7, Alves 7, Pique 6.5, Mascherano 6.5, Alba 6, Rakitic 6, Busquets 7, Iniesta 7, Messi 8, Suarez 6.5, Neymar 7.
Messi akipiga mpira unaompita kipa Petr Cech na kuwa bao la kwanza kwa Barcelona
Messi akifunga bao la pili kwa mkwaju wa penalti
Namba 9 wa Barcelona Luis Suarez akisikitika baada ya kukosa bao la wazi
Comments
Post a Comment