BARCELONA            inapanga kuizidi kete Chelsea kwa kumsajili winga wa kimataifa            wa Algeria anayekipiga Leicester City, Riyad Mahrez kwa dau la            pauni milioni 23.
        Mwarabu huyo mwenye umri wa miaka 25,            amekuwa na kiwango cha juu akiwa na vinara hao wa Premier            League aliowafungia mabao 15 na kupika mengine 10 msimu huu.
        Gazeti la Daily Star limesema kuwa Chelsea            inaangalia uwezekano wa kunasa saini ya winga huyo ambaye            anatajwa kumvutia mmiliki wa klabu hiyo, Roman Abramovich,            lakini sasa rpoti kutoka Hispania zinapasha kwamba Barcelona            nayo imejitosa katika dili hilo na kuachana na mipango ya            kumtwaa mshambuliaji wa Celta Vigo, Nolito.
        Barca ilipeleka maombi mara kadhaa kwa            ajili ya mshambuliaji huyo Mhispania bila mafanikio, na sasa            imeamua kugeuzia mipango yake kwa Mahrez ambaye kasi yake na            maamuzi ya haraka vimemshawishi Luis Enrique kwamba anafiti            katika safu yake ya mashambulizi.
        Mahrez alitua England mwaka 2014 akiwa si            mchezaji wa kujulikana, akitoka kuitumikia kwa miaka mine            klabu ya Le Havre ya Ufaransa.
        
Comments
Post a Comment