Luis Suarez na Neymar wamefunga kwa mara nyingine tena na kuiongoza Barcelona kushinda 2-1 kwenye mchezo wa La Liga dhidi ya Las Palmas.
Ushindi huo unafanya Barcelona izidi kutanua rekodi yake hadi kufikia mechi 32 bila kupoteza mchezo.
Suarez alifunga katika dakika ya sita tu huku Neymar akifunga kabla ya mapumziko hiyo ikiwa ni baada ya Willian Jose wa Las Palmas hajafanya matokeo yasomeke 1-1.
Luis Suarez akipongezwa baada ya kuifungia Barcelona bao la kwanza
Comments
Post a Comment