ARSENE Wenger ana matumaini kuwa rekodi ya kipa wake Petr Cech dhidi ya Lionel Messi itamnyamazisha staa huyo wa Barcelona watakapokutana katika mechi ya awali ya Ligi ya Mabingwa hatua ya 16 bora leo usiku.
Mshambuliaji huyo raia wa Argentina hajafanikiwa kumfunga kipa huyo wa kimataifa wa Jamhuri ya Czech katika mechi nane zilizopita na Wenger anaamini rekodi hiyo itamchanganya Messi kiasi cha kushindwa kutekeleza wajibu wake kisawasawa dimbani.
Messi amejipambanua kuwa mchezaji bora zaidi duniani na Cech atahitaji kuwa katika ubora wake kuweza kumtuliza.
Wenger anaukubali 'muziki' wa Barcelona linapokuja suala la mashambulizi na kwamba hajaona machezaji mwenye rekodi ya kutisha kama Messi, lakini anaamini kuwa historia iko upande wao dhidi ya staa huyo.
Comments
Post a Comment