ARSENAL inatarajiwa kufanya mazungumzo na Mkurugenzi wa Inter Milan, Pietro Ausilio wiki hii kuhusu dili la usajili wa kiungo wa klabu hiyo ya Italia, Marcelo Brozovic.
The Gunners walihusishwa kwa kishindo na dili la kumsajili Brozovic mwezi Januari, huku Arsene Wenger akitajwa kuwa shabiki mkubwa wa kiungo huyo.
Gazeti la Tuttosport limeandika kuwa Ausilio atapanda ndege kwenda London wiki hii kujadili biashara ya kumuuza kiungo huyo kwa Arsenal.
Kwa sasa Brozovic anaichezea Inter kwa mkopo akitokea Dinamo Zagreb ya nyumbani kwao Croatia, lakini miamba hiyo ya Serie A ina chaguo la kumpa usajili wa moja kwa moja kabla ya kumpiga bei.
Arsenal inaweza kulipa pauni milioni 15.6 kwa ajili ya kiungo huyo, ambaye Inter iko tayari kufanya biashara ili kutunisha mfuko wake.
Comments
Post a Comment