UONGOZI wa Yanga, umeeleza kwamba wakati wowote unaweza kuamua kutumbua jipu kama anavyofanya rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, John Pombe Magufuli kwa kuanika wanaoihujumu.
Kauli hiyo imetolewa na Mkurugenzi wa Mawasiliano wa klabu hiyo, Jerry Muro wakati akizungumza na Saluti5 na kufafanua kuwa wapo mbioni kufanya hivyo kutokana na kuwapo hali ya kutaka kuzibeba baadhi ya timu.
Alisema, wamegundua timu hizo zimekuwa zinabebwa na viongozi ambao wapo ndani ya Shirikisho la Soka nchini (TFF), ili kuzipa nafasi baadhi ya timu kutokana na wao kupangiwa kucheza mechi huku timu nyingine zikisubiri.
"Tunajua wazi kwamba sisi tunapangwa kucheza kwanza huku wenzetu wanaangalia nini tunafanya bila wao kucheza, hapo kuna kasoro ukweli tutauweka wazi kama anavyotumbua majipu rais wetu Magufuli," alisema Muro.
Comments
Post a Comment