Hatimaye kocha wa Chelsea Jose Mourinho ametimuliwa kazi baada ya mwenendo mbovu msimu huu.
Sasa Roman Abramovich atalazimika kumlipa Jose Mourinho zaidi ya pauni milioni 40 ikiwa ni mshahara wake wa sehemu iliyobakia kwenye mkataba wake uliovunjwa.
Abramovich, tajiri wa Kirusi anayemiliki Chelsea, aliongoza kikao cha bodi ya timu akiwa na menejimenti yake - Bruce Buck, Marina Granovskaia, Eugene Tenenbaum na Michael Emenalo — ambapo iliamuliwa Mourinho atimuliwe.
Kuunununua mkataba wake wa miaka minne wenye thamani ya pauni 250,o00 kwa wiki, ni ilikuwa ni moja ya sababu kubwa za kushindwa kumtimua Mourinho mapema, mara tu baada ya kusaini mkataba huo mpya.
Mourinho alikubabali kusaini mkataba mpya mwishoni mwa mismu uliopita na ilipofika mwezi Agust klabu ikatangaza rasmi mkataba huo wa miaka minne wa kocha huyo wa Kireno.
Baada ya kushinda taji la Premier League kiulaini msimu uliopita, Chelsea ikaamini kuwa Mourinho ni kocha bora duniani na ikampa moja kwa moja mkataba mpya wa miaka minne bila kuweka kipengele cha manunuzi ya mkataba huo iwapo klabu hiyo ingeamua kumtimua.
Mwaka 2007 Septemba, alimlipa Mourinho na benchi lake la ufundi pauni milioni 16 pale alipomtimua ingawa baadae alimtumia kocha huyo gari la kifahari aina ya Ferrari kama shukrani kwa kazi yake aliyoifanya Chelsea.
Comments
Post a Comment