Wolfsburg vs Man United: Van Gaal Hajawahi Kupoteza Mechi vs Wolfsburg, United Inatakiwa Kushinda Tu Ili Kufuzu
VfL Wolfsburg na Manchester United FC zinakutana leo kwenye mechi ya sita ya hatua ya makundi huku timu zote zikitaka matokeo chanya ili kujihakikishia nafasi ya kufuzu hatua ya mtoano wa UEFA Champions League.
Tuangalie mambo mbalimbali yanayohusu mechi hii
- Wolfsburg watakuwa wamefuzu endapo watapata sare tu na watakuwa wamejihakikishia nafasi ya kwanza kwenye kundi.
- United, wakiwa nyuma kwa pointi moja ya Wolfsburg, wanahitaji kushinda ili nafasi ya kufuzu.
- United hawajafungwa katika mechi 11 zilizopita, lakini ni mechi 4 tu kati ya hizo ndio walipata ushindi.
- Wayne Rooney, atakuwa nje ya dimba kutokana na majeruhi ya enka.
- Wajerumani hawajawahi kufika raundi ya 16 bora ya UEFA – Hii ndio mara yao ya pili kushiriki kwenye michuano hii.
- Mechi ya mwisho ya nyumbani ya Wolfsburg dhidi ya timu ya England ilikuwa ya kipigo cha 2-0 dhidi ya Everton FC katika msimu uliopita wa UEFA Europa League group stage.
- Mechi ya kwanza ya Wolfsburg dhidi ya timu za England, ilikuwa ya ushindi wa 3-2 dhidi ya Portsmouth FC katika 2008/09 UEFA Cup hatua ya makundi. Tangu wakati huo wamepoteza mechi 7 mfululizo dhidi ya timu za England.
- Timu ya Old Trafford ilikutana na kisanga kama cha leo usiku katika msimu wa 2011/12 baada ya kufungwa 2-1 defeat na FC Basel 1893 katika mechi ya mwisho ya makundi. David de Gea, Phil Jones, Smalling, Wayne Rooney na Ashley Young wote walicheza mchezo huo ambayo ilichezwa 7 December 2011.
- Rekodi ya Manchester United dhidi ya vilabu vya Ujerumani – ni ushindi wa mechi 5, sare 4, na wamefungwa 5.
JE WAJUA?
Van Gaal hajawahi kupoteza mechi yoyote dhidi ya Wolfsburg wakati alipokuwa Bayern, akishinda mechi zote 4 alizokutana nayo.
VIKOSI VINAVYOWEZA KUANZA LEO
Wolfsburg: Benaglio; Träsch, Naldo, Dante, R Rodríguez; Arnold, Guilavogui/Luiz Gustavo; Vierinha, Draxler, Caligiuri; Dost.
Out: Felipe (foot), Knoche (ankle)
Doubtful: Luiz Gustavo (back)
United: De Gea; McNair, Smalling, Blind; Young, Carrick, Schweinsteiger, Mata, Darmian; Depay, Martial.
Out: Rooney (ankle), Schneiderlin (hip), Jones (ankle), Herrera (hamstring), Valencia (foot), Rojo (shoulder), Shaw (broken leg)
Doubtful: McNair (ankle)
Comments
Post a Comment