Kocha wa Arsenal Arsene Wenger amefichua kuwa ushindi            dhidi ya Man city imepiga jeki imani wanayohitaji katika mbio            za kutwaa ligi ya Uingereza msimu huu.
        Arsenal haijawahi kunyanyua taji hilo tangu mwaka wa            2004.
        Hata hivyo mabao ya Theo Walcott na Olivier Giroud            yalitosha dhidi ya Man City.
        The Gunners walijifurukuta na kuwanyamazisha City mbele            ya mashabiki wa nyumbani .
        Licha ya bao la Yaya Toure Man City hawakuweza kuizima            Gunners ambao walikuwa wakitafuta alama tatu muhimu na            kupunguza pengo la alama kutoka kwa vinara wa ligi hiyo            Leicester.
        "Inatupa ujasiri, nguvu na," alisema Wenger, mwenye            umri wa miaka 66.
        "Kikosi kimeonyesha ukomavu ambao ungeweza kushuhudia            katika mchuano tulipokuwa na shinikizo la kufanya vyema."
        Arsenal inaoongoza city kwa alama 4 lakini bado wako            alama mbili chini ya vinara Leicester City.
        Huku mabingwa watetezi, Chelsea wakiwa nje ya mbio za            kuwania taji la ligi, mababe hao wa kusini mwa London ndio            wanaopigiwa upatu kuibuka washindi wa ligi.
        Arsenal haijapoteza mechi 6 na ushidi wao katika mechi            tano kati ya mechi zake sita umewawezesha kuchupa hadi nafasi            ya pili msimu wa krismasi.
        "Miaka miwili au mitatu iliyopita, tuliongoza kwa            kipindi kirefu lakini uzuri wa wakati huu ni kuwa tumepoteza            wachezaji bora, tulicheza dhidi ya Olympiakos, Villa na leo,            tumeshinda mechi zote," alisema Wenger.
        "Ni ishara nzuri. Naamini tumeonyesha uwezo wetu,            matayarisho, na uhodari kwa jumla na imetupa alama tatu.
        "Wakati tulikuwa tumechoka tulitegemea matumaini na            hilo limetuwezesha tumalize katika nafasi nzuri."
        Harakati za dakika za mwisho za City zilizoongozwa na            Toure hazikutosha kuilemaza Arsenal.
        City walionekana kupungukiwa ushupavu wao ugani            Emirates bila beki wao wa kutegemewa, Vincent Kompany na            Sergio Aguero aliyepata afueni baada ya kuuguza jeraha.
        "Ilikuwa muhimu kwa Sergio kurudi kwa timu ,labda            anahitaji mechi kadhaa kurejea katika fomu yake," alidai            Pellegrini.
        "Kuna alama 63 za kushindaniwa , mechi kadhaa na            tulivyocheza katka kipindi cha pili inaonyesha tunazidi            kushindania ligi."
        City wamepoteza mechi tano msimu huu na timu ya mwisho            kupoteza mechi tano kabla ya Krismasi na kushinda ligi ilikuwa            Everton kati ya mwaka wa 1986-87.
        Hata hivyo Pellegrini amesema kuwa; "Sijui takwimu            lakini hatuko nje ya mbio za kushinda ligi. Ikiwa hauamini ,            hauko katika taaluma."
        
Comments
Post a Comment