Alexis Sanchez amepata kikwazo cha kurejea uwanjani wakati akielekea kupona maumivu yake ya msuli wa paja na sasa kocha wa Arsenal, Arsene Wenger amesema nyota huyo atarejea kikosini mwezi Januari.
Mshambuliaji huyo ambaye aliumia katika mchezo wa sare ya 1-1 dhidi ya Norwich mwezi uliopita, alitarajiwa kuwa kwenye kikosi cha Arsenal kilichoichapa Manchester City 2-1 Jumatatu usiku, lakini sasa mambo yamwekwenda kombo kwake.
Baada ya mchezo huo wa Premier League dhidi ya City, Wemger alisema: "Nadhani Sanchez atarejea uwanjani Januari 10. Amepata vikwazo kidogo siku mbili zilizopita. Tulitarajia angekuwa kwenye benchi leo (jana) usiku".
Alexis Sanchez (pichani katikati) akifuatilia mchezo wa Arsenal na Manchester City
Sanchez aliumia msuli wa paja katika mechi ya forward 1-1 dhidi ya Norwich mwezi uliopita
Wenger alikuwa na matumaini kuwa Sanchez angecheza dhidi ya Man City Jumatatu usiku lakini sasa mshambuliaji huyo atarejea uwanjani mwezi Januari
Sanchez ameichezea Arsenal mechi 20 msimu huu na kufunga magoli 9
Comments
Post a Comment