WAKALA wa mchezaji mahiri wa timu ya soka ya Manchenster United ya nchini Uingereza, Wayne Rooney, amesema kwamba mchezaji huyo hana mpango wa kutaka kutua nchini China kama inavyoripotiwa.
Taarifa iliyotolewa na wakala huyo, imeeleza kwamba mchezaji huyo hajawahi kukutana na viongozi wa timu yoyote ya nchini humo na kueleza kwamba bado ana mkataba wa kuitumikia Manchester United.
Aliema yeye kama msimamizi wa mchezaji huyo, hana taarifa yoyote ya mkali huyo kutakiwa nchini China kama inavyoripotiwa katika baadhi ya vyombo vya habari.
Majuzi iliripotiwa kuwa klabu ya Shanghai SIPG inayonolewa na kocha za zamani wa England Sven Goran Eriksson imetenga pauni milioni 75 ili kumnasa Rooney.
Katika habari hizo, ikadaiwa kuwa klabu hiyo ipo tayari kumpa Rooney mkataba wa miaka mitatu wenye thamani ya pauni milioni 25 kwa msimu.
Rooney kuungana tena na Sven Goran Eriksson?
Comments
Post a Comment