“WACHEZAJI WASILAUMIWE KUFUKUZWA KWA MOURINHO”…


"WACHEZAJI WASILAUMIWE KUFUKUZWA KWA MOURINHO"…

momo

Mara baada ya kutimuliwa kazi kuwa meneja wa Chelsea Jose Mourinho, mkurugenzi wa soka wa Chelsea, Michael Eminalo amesema wachezaji hawatakiwi kutupiwa lawama kwa yaliyomtokea Jose Mourinho.

Ingawa Eminalo hakutaja jina la kocha Mourinho katika kikao chake na waandishi wa habari, alisisitiza kuwa siku zote wachezaji sio sababu ya kufukuzwa kwa meneja wao, huku asitaje jina la Jose Mourinho.

Emilano amesema kuwa sababu za kufukuzwa kwa kocha Jose Mourinho zipo wazi kwani timu haipati matokeo stahiki wakati timu ni ile ile iliyochukua ubingwa miezi sita iliyopita na sasa wachezaji hawana morali.

Chelsea iko katika nafasi ya 16 pointi 1 tofauti na timu iliyokatika mstari wa kushuka daraja huku wakiwa na points 15 na kupokea vipigo 9 hadi sasa, wakishinda michezo 4 pekee na kupata sare 3, kikosi kile kile kilichotwaa ubingwa miezi sita iliyopita.

Kufukuzwa huko kwa Mourinho kumezua majadiliano makubwa duniani kote ambapo asilimia kubwa ya wachambuzi na mashabiki wa soka wamesikitishwa na kufukuzwa kwa kocha huyo, ambaye ni bora zaidi kuwahi kuifundisha Chelsea.

Kabla ya kufukuzwa wiki iliyopita kocha huyo mara baada ya kumalizika kwa mchezo waliopoteza kwa goli 2-1 dhidi ya Leicester, alisema kuwa wachezaji wanamsaliti kwa kutotekeleza maagizo yake anayoyatoa mazoezini na ndio sababu wamekua hawapati matokeo.



Comments