WACHEZAJI WA MANCHESTER UNITED WALIVYOTINGA MAZOEZINI NA MAGARI YAO YA KIFAHARI 'KUAGANA' NA VAN GAAL
Wakiwa na nyuso za huzuni kufuatia kipigo chao cha wikiendi iliyopita cha bao 2-1 kutoka kwa Norwich City, wachezaji wa Manchester United waliwasili mazoezini Jumatatu huku ikiaminika kuwa siku za kocha Louis van Gaal zinahesabika.
Kocha huyo ambaye duru za michezo zinaamini kuwa atatimuliwa kabla ya mwaka mpya, anatarajiwa kurithiwa na Jose Mourinho aliyefukuzwa Chelsea.
Mastaa wa United waliozomewa Jumamosi baada ya mchezo wa Norwich, wakatinga mazoezini ma magari yao ya kifahari lakini wakiwa na sintofahamu juu Van Gaal ambaye amekuwa akishutumiwa kwa falsafa zake.
Gazeti la The Sun la Uingereza limeandika kuwa kuna tetesi kwamba Mourinho amefanya mazungumzo na Manchester United na sasa kinachosubiriwa ni matajiri wa familia ya Glaizer inayomiliki United kutoa tamko la kumtema Van Gaal.
Je mazoezi ya wachezaji wa Manchester United wiki hii yatakuwa ndio ya kuagana na Van Gaal au ni uzushi mtupu? Ni jambo la kusubiri.
Memphis Depay akitinga na Mercedes G-Class yenye thamani ya pauni 87,795 ambayo kwenye viegemeo vya kichwa imeandikwa M7 kumaanisha jina lake na namba ya jezi yake
Chris Smalling
Marouane Fellaini
Wayne Rooney na Range Rover Overfinch yenye thamani ya pauni 100,000
Blind akiwasili na Audi Quattro
Ashley Young
Louis van Gaal safari ya kuondoka United inanukia
Comments
Post a Comment