VITA 3 MUHIMU, MAN UNITED KUUVUKA MLIMA WA WOLFSBURG LEO?



VITA 3 MUHIMU, MAN UNITED KUUVUKA MLIMA WA WOLFSBURG LEO?

who 3

Na Simon Chimbo

Manchester United leo usiku itakua ikipambana na klabu ya soka ya VfL Wolfsburg katika uwanja wa nyumbani wa VfL, Volkswagen Arena katika mchezo wa mwisho wa klabu bingwa Ulaya hatua ya makundi. Wolfsburg ndio vinara wa kundi wakiwa na points 9 wakifuatiwa na Manchester United points 8, PSV Eindhoven points 7 na CSKA Moscow points 4.

Katika kujihakikishia kufuzu hatua inayofuata ya 16 bora, Manchester United hawana kingine wanachostahili kufanya bali ushindi, ni mlima mrefu, hasa ukizingatia kuwa PSV ana asilimia kubwa ya kuwafunga vibonde CSKA Moscow tena PSV wakiwa nyumbani kwao Uholanzi.

Sare haiwasaidii kitu Manchester United, ambayo imesafiri bila ya nahodha wake Wayne Rooney ambaye jana alionekana katika dimba la Goodson Park uwanja wa nyumbani wa Everton kutizama mechi kati ya Everton na Crystal Palace, mshambuliaji huyo bado ni majeruhi, na sasa timu inahitaji matokeo ya ushindi.

Yafuatayo ni maeneo muhimu matatu ambapo United inahitaji kushinda ili kuibuka na ushindi leo usiku;

1. DANTE vs ANTHONY MLARTIAL

Wayne Rooney hayupo, Anthony Martial atakua akiongoza mstari wa ushambuliaji wa timu hii. Kikubwa hapa ni kwamba kasi na wepesi 'pace' wa Anthony Martial atakua muhimu zaidi dhidi ya Dante ambaye hana kasi kabisa na hakika kama Martial akiwa na usiku mzuri, ataweza msumbua sana Dante ambaye amekosa pace.

Tofauti na ilivyokua dhidi ya Westham, Anthony Martial alipata wakati mgumu kupenya mbele ya mlinzi Winston Reid, lakini kwa Dante haitokua kazi kubwa kwa beki ambaye mara ya mwisho aliichezea Brazil katika kipigo cha goli 7-1 toka kwa Ujerumani kombe la dunia 2014.

2. JULIAN DRAXLER vs BASTIAN SCHWEINSTEIGER

Uzoefu wa kiungo Bastian Schweinsteiger katika michuano kama hii unaweza kuisaidia United leo pale atakapoweza mdhibiti kiungo mjanja mjanja Julian Draxler.

Schweinsteiger ni mwenyeji wa Ujerumani, anamjua vizuri Draxler na ni aina ya wachezaji wanaoweza kutimiza majukumu yao wakiwa uwanjani.

3. BAS DOST vs CHRIS SMALLING

Huu ni msimu mzuri sana kwa mlinzi Chris Smalling ambaye bila shaka leo atawaongoza wenzake uwanjani Wayne Rooney akiwa hayupo. Amekwisha pambana na washambuliaji wengi wazuri hadi sasa, na uwezo wake msimu huu hautii shaka kwamba anaweza mtuliza mshambuliaji huyu wa Wolfsburg, Bas Dost asifurukute.

Lakini Smalling anahitaji kuwa katika fomu yake kumdhibiti Draxler ambaye ameshafunga magoli 9 msimu huu. Urefu wake wa futi 6.5 ni mtihani mwingine kwa Smalling ambaye atatakiwa kuwa vizuri kutokana uhatari wa Draxler katika mipira ya juu.



Comments