KLABU ya Manchester United imeendelea kufanya vibaya katika Ligi Kuu ya England, lakini kocha wake Louis Van Gaal anasema hawatakata tamaa.
Kocha huyo raia wa Uholanzi aliyasema hayo baada ya juzi kupigwa mabao 2-1 na timu ya Bournemouth.
Kipigo hicho kimewafanya United waendelee kuganda nafasi ya nne katika msimamo lakini wakiwa pointi nne tu nyuma ya vinara wa Ligi hiyo, Arsenal.
"Inaumiza na kuvunja moyo kupoteza mechi mbili mfululizo lakini hatutakata tamaa ya ubingwa kwasababu kimsimamo bado hatujashuka sana, ni suala la kujipanga na kupambana kwa nguvu zaidi," aisema Van Gaal.
Aliema atahakikisha kikosi hicho hakiruhusu tena kupoteza mchezo wowote katika kipindi hiki cha mechi nyingi za sikukuu ya Krismasi na Mwaka Mpya, ambacho ndicho huwa kigumu kwa kila timu.
Louis Van Gaal amewahakikishia mashabiki wa klabu hiyo kuwa, hawatatoka mikono mitupu msimu huu.
Comments
Post a Comment