KOCHA wa Manchester United, Louis Van Gaal ni kama amewaponda kiaina washambuliaji wake akiwamo nahodha Wayne Rooney.
Van Gaal alisema juzi kuwa, anaamini timu hiyo ingekuwa kileleni mwa Ligi Kuu kama ingekuwa na mshambuliaji mahiri wa Uruguay Luis Suarez au staa wa Argentina na wapinzani wao, Manchester City, Sergio Aguero.
Kocha huyo mwenye miaka 64 raia wa Uholanzi, aliyasema hayo kwa hasira baada ya vijana wake kubanwa na kulazimishwa sare ya bila mabao na West Ham United kwenye dimba lao la Old Trafford mwishoni mwa wiki.
"Ninaamini tungekuwa na watu kama Sergio Aguero au Luis Suarez kwa sasa tungekuwa na mabao mengi," alisema.
Aliwaponda Wayne Rooney na Memphis Depay kuwa hadi sasa Ligi ikiwa mzunguuko wa 15 kila mmoja ana mabao mawili pekee.
Alisema, timu kuwa na washambuliaji wanaozidiwa mabao na viungo ni ngumu kufanikiwa ambapo aliwafagilia viungo Anthony Martial mwenye mabao manne.
"Watu wananiuliza, hivi tungekuwa na washambuliaji wengine tungekuwa tunafunga?, mimi nasema kama tungekuwa na Luis Suarez au Sergio Aguero tungepata mabao kila mechi," alisema kuiambia BBC Radio Manchester.
Van Gaal yuko mwenye mkakati mgumu wa kupigania ubingwa au nafasi nne za juu zitakazompa tiketi ya kucheza Ligi ya Mabingwa Ulaya mwakani.
Comments
Post a Comment