Van Gaal Amepoteza Haki ya Kuamua Ataondoka Vipi Old Trafford


Van Gaal Amepoteza Haki ya Kuamua Ataondoka Vipi Old Trafford

Kwanza ni muhimu kuliweka hili wazi, kwa namna inavyoonekana na kutokana na utaratibu wao katika uajiri na kufukuza, pamoja na kuendelea kufanya vibaya bado hakuna hamu ya kumfukuza Louis van Gaal Old Trafford, angalau kwa sasa. 

  Ameshafanya kwa asilimia kubwa kile alichotakiwa kufanya. Ameipanga upya United. Ameboresha matokeo ya nyumbani na aliweza kuirudisha timu kwenye Champions League hata kama kwa muda mfupi. Pia amewaweka kwenye nafasi ya kushindania ubingwa wa premier league msimu huu. 

Lakini hawezi kuepukana na lawama juu ya kufeli kuvuka hatua ya makundi ya Champions League katika kundi lenye timu za Wolfsburg, PSV Eindhoven na CSKA Moscow – hili linaonyesha kufeli kwa mdachi huyo..

Na mpaka kufikia sasa, ameshapoteza haki ya kuamua namna na lini muda wake ndani ya Old Trafford utafikia kikomo. 

Van Gaal ameshaongelea hatma yake huku akionekana kuwa na uhakika wa hatma yake – anaonekana kuwa na control ya kilicho mbele yake. Anaongelea mipango ya kumaliza miaka yake mitatu ya mkataba na kisha kustaafu katika 'paradise' nchini Portugal na mkewe, Truus.

  
Lakini wapo mamilioni ya mashabiki wa United ambao wanaoamini kwamba Van Gaal hajafanya kazi ya kutosha ya kumpa haki ya kuamua namna na muda wa kuondoka. Sir Alex Ferguson aliyefanya makubwa ya kumpa haki , lakini sio Louis.

 Wakati Gary Neville alipokuwa nahodha wa United, mara zote alikuwa akisisitiza kupeana mikono kabla ya mechi na kauli yake maarufu 'hapa Old Trafford tunapeana mikono, na sio vinginevyo vyovyote'. Na katika namna hiyo hiyo pia, klabu yenye ukubwa size ya United inakuambia muda wa kuondoka na namna ya safari yako itakuwa na sio vinginevyo vyovyote.

Maneno haya yote yanaweza kuwa kelele tu zisizo za msingi, lakini kuna nafasi kubwa angalau msimu ujao kutakuwa na jambo mbadala.  

Carlo Ancelotti anataka kazi mpya kuanzia msimu ujao
 

Carlo Ancelotti tayari ameshasema anataka kurejea kufundisha, na labda katika premier league. Pep Guardiola atakuwa kamaliza mkataba mwishoni mwa msimu. Ikitokea siku Roman Abramovich akaamka vibaya , Jose Mourinho nae atakuwa hana kazi. Antonio Conte na Diego Simone nao pia wanaweza kuwemo katika listi.

Wote hawa wana ubora na kasumba zao, lakini wote kwa sasa wanaweza kuwa wabadala sahihi kwa Van Gaal.

Pamoja na matokeo mabaya ya timu, kuna asilimia kubwa mdachi huyu atamaliza msimu akiwa kocha wa United. Lakini kitakachojiri kuanzia sasa na mbeleni kitaamua hatma yake baada ya msimu kuisha.   
Ikiwa United watashinda ubingwa au wakawa nafasi ya pili na kushinda FA Cup, hapo mashabiki wengi watakubali anastahili kuendelea kubaki.

Lakini itakuwaje kama United watamaliza nafasi ya 4 na kumaliza msimu wa tatu bila kushinda kombe lolote? 

Wataendelea kubaki na Van Gaal kwa mwaka mwingine wakati Ancelotti na Guardiola wakienda sehemu nyingine? Na Je hii inamaanisha United watabakia kuchukua kocha kutoka kwenye kundi la pili wakati Van Gaal mkataba wake utakapoisha? Labda wamchague Ryan Giggs ambaye kiuhalisia bado hajawiva kuwa kocha wa timu yenye ukubwa wa United, hata Gary Neville pia. 

Kama ilivyo staili ya soka lake na matumizi ya 
 £258m alizotumia kwenye usajili, kuondolewa kwenye UCL kwa namna walivyoondolewa na  Wolfsburg jumanne usiku hakutamsaidia lolote Van Gaal.
 

Van Gaal ametumia zaidi ya £200m kwenye Usajili
 

Mashabiki watakumbuka kwamba wakati United inahitaji goli, LVG akawaingiza Micheal Carrick na Nick Powell kwa sababu ameshauza au kuwatoa kwa mkopo washambuliaji wake.

Pia watakumbuka, kwamba alisema kuendelea kucheza hatua moja mbele katika Capital One Cup msimu huu kunaonyesha maendeleo kutoka msimu uliopita alipoanza kazi. Hii ni kauli isiyoendana na hadhi ya United.

Kwa mara ya kwanza Van Gaal amepoteza control ya maamuzi juu ya lini na namna gani  ataondoka Old Trafford. Lakini huu sio uhusiano ambao haujafikia hatua ya kutoutengeneza upya. Lakini amesababisha mwenyewe kuanza kukimbizana na vivuli vya Ancelotti na Guardiola. 



Comments