TP – MAZEMBE INAVYOFAIDIKA NA UWEKEZAJI WA MOISE KATUMBI


TP – MAZEMBE INAVYOFAIDIKA NA UWEKEZAJI WA MOISE KATUMBI
Ndege inayomilikiwa na klabu ya TP Mazembe kwa ajili ya              safari za klabu hiyo
Ndege inayomilikiwa na klabu ya TP Mazembe kwa ajili ya safari za klabu hiyo

Kitu kingine kikubwa ambacho Samatta amekieleza katika safari yake ni pamoja na namna ambavyo klabu ya TP Mazembe inavyonufaika na uwekezaji mkubwa wa bilionea Moise Katumbi.

Katumbi ameijengea Mazembe uwanja mpya wa kisasa wenye hadhi ya kimataifa na ambao unaruhusiwa na FIFA kuchezewa michezo ya kimataifa. Lakini pia Katumbi amenunua ndege binafsi ambayo hutumiwa na klabu hiyo katika safari zake binafsi ili kurahisisha usafiri wa timu hiyo pale inapotakiwa kusafiri safari ndefu.

Ile ni ndege binafsi ya klabu na ameinunua yule bosi kwa pesa zake, si kwamba amepewa waitumie kwa muda flani, ni yeye mwenyewe ameinunua hiyo ndege isaidie timu itakapokuwa inasafiri.

TP Mazembe 4

TP Mazembe historia yake ni kama timu ya kifamilia, kabla ya Moise Katumbi kulikuwa na kaka yake ambaye alikuwa anaimiliki hiyo timu. Lakini kakayake aliingia kwenye mambo ya kisiasa lakini historia ya kisiasa nchini Congo DR siyo nzuri, baada ya kuingia kwenye masuala ya kisiasa ikatokea mambo ya kutishana na wanasiasa ikabidi jamaa aondoke hadi sasa anaishi Ulaya kwahiyo baada ya kuondoka akamwahia timu mdogoake ambaye ndiyo Moise Katumbi.

Kwahiyo TP Mazembe ni timu ya mtu binafsi ambaye anatoa pesa zake mfukoni anaweka kwenye timu.



Comments