Takwimu Mbaya Zaidi Kwenye EPL – Manchester United Yaongoza



Takwimu Mbaya Zaidi Kwenye EPL – Manchester United Yaongoza

Msisitizo wa Manchester United kucheza soka la kumiliki mpira zaidi chini ya kocha Louis van Gaal umefanya wawe wanapiga pasi nyingi zaidi kabla ya kupiga mpira langoni kwa adui kuliko timu yoyote kwenye Premier League, takwimu ziliztolewa jana jumatatu zimeonyesha.

Kwa mujibu wa OPTA, viongozi wa ligi hiyo Leicester City wanahitaji pasi zisizozidi 46 ili kufanikiwa kupiga shuti langoni, idadi chache zaidi kwenye ligi wakati United wakishika nafasi ya kwanza kwa kuhitaji kupiga pasi zisizozidi 131 kabla ya kufanikiwa kupiga shuti moja langoni.

Van-GaalKibaya zaidi, United wamefanikiwa kupiga mashuti saba tu yaliyolenga goli katika mechi zao nne zilizopita katika uwanja wao wa nyumbani – rekodi mbaya zaidi kwenye ligi – ambayo imepelekea mashabiki wake kuimba wimbo wa "attack, attack, attack".

Idadi ya mashuti yaliyolenga goli katika mechi zote 17 za ligi ni 61, idadi hii inawafanya washike nafasi ya 15 kwenye kwa kupiga mashuti machache yaliyolenga goli. Tottenham wanaongoza kwa mashuti 110 na Manchester City wakifuatia na mashuti 104.

JS59212401Katika iezi miwili iliyopita United wamecheza mechi tano zilizoisha kwa sare tasa ya 0-0 katika dimba la Old Trafford, dhidi ya Manchester City, Middlesbrough, CSKA Moscow, PSV Eindhoven na West Ham.

Kisichongaza, jumla ya magoli waliyofunga ni ndogo sana – wamefunga magoli 22, kulinganisha na 43 katika hatua kama hii ya msimu chini ya utawala wa Alex Ferguson misimu mitatu iliyopita. Chini ya Van Gaal msimu uliopita walikuwa na magoli 30, lakini wakiwa wameruhusu magoli mengi zaidi. Lakini kocha msaidizi wakati wa utawala wa Moyes, Steve Round, anasema: "Wanancheza mchezo wa kumiliki sana mpira, ndio maana wanatengeneza nafasi chache. Mara zote nilikuwa nahisi wanancheza kwa utamaduni wa kupiga pasi kweneye mbele zaidi, hii ndio ilikuwa style yao, huku wakiongezea nguvu na kasi, lakini sasa wameondokana na utamdauni huo.Manchester-United-vs-Tottenham

"Staili wanayocheza ni mfumo wa wa Louis van Gaal. Tutaona kama utaleta manufaa huko mbele, ni suala la kusubiri."

Kupoteza 2-1 nyumbani dhidi ya Norwich City jumamosi iliyopita, ilikuwa mechi yao ya sita mfululizo kucheza bila kushinda na hivyo wakapoteza nafasi yao kwenye top 4.

Matokeo mabaya yamezidi kumpa presha Van Gaal miezi mitano baada ya mwaka wake pili kwenye mkataba wake wa miaka 3 – na sasa inaaminika endapo atapoteza mchezo dhidi ya Stoke City Jumamosi basi atatimuliwa na huenda Jose Mourinho au Pep Guardiola wakamrithi.



Comments