WAKATI klabu kadhaa zikionekana kummezea mate Luis Suarez FC Barcelona, mpiga mabao huyo amesema kwamba ana furaha isiyo kifani kuwa hapo kuliko kwenye timu nyingine yoyote barani Ulaya.
Suarez amesema hafikirii kuondoka Barcelona kwa vile hiyo ni klabu kubwa duniani lakini pia La Liga ndiyo ligi bora kuliko zingine zote.
Alieleza kwamba miongoni mwa vitu ambavyo vimekuwa vinamfanya aipende La Liga, ni ushindani kuanzia kwa wachezaji hadi timu sambamba na hamasa za mashabiki.
"Mashabiki wamekuwa chachu ya mafanikio yangu ndani ya uwanja, sio siri kwamba nikiendelea kuwapo ndani ya timu hii nitapata mafanikio makubwa," alisema nyota huyo ambaye alitua Barca akitokea timu ya Liverpool ya Uingereza na kuongeza: "Unaanzaje kufikiria kuondoka Barcelona?"
Majuzi Suarez alipata tuzo ya dhahabu baada ya kuwa mfungaji bora wa Klabu Bingwa ya Dunia na kuisaidia Barcelona kutwaa taji hilo mbele ya River Plate ya Argentina.
Comments
Post a Comment