KOCHA mpya wa klabu ya Valencia ya Hispania, Gary Neville (pichani juu), amemwagiwa sifa na kocha wa zamani wa Manchester United, Sir Alex Furguson kuwa ni mwenye bahati katika medani hiyo.
Neville alianza kazi ya kuinoa Valencia mwanzoni mwa juma hili baada ya mechi ya sare ya 1-1 na Barcelona, akishuhudiwa na mamia ya mashabiki wa klabu hiyo.
Akizungumza katika mkutano wa Tech Crunch Disrupt, jijini London, Fergie alisema kila anachogusa Gary Neville hubadilika na kuwa dhahabu.
Fergie alisema, Neville amekuwa mtu ambaye inakuwa vigumu kuamini anachokifanya kwani amekuwa akifanya vizuri katika kila sekta.
Aidha, Fergie alisema hata alipokuwa kwenye uchambuzi katika luninga, amekuwa wa kustaajabisha na kwamba hata sasa katika klabu hiyo ya Valencia atapata mafanikio.
Neville alitoa maisha yake kwa kocha Fergie kwa miaka 19 akitwaa mataji mengi na akiitumikia timu ya taifa mechi 85.
Comments
Post a Comment