SIKU ZA LOUIS VAN GAAL ZAHESABIKA MANCHESTER UNITED NORWICH IKIFANYA KITU MBAYA OLD TRAFFORD ...Jose Mourinho ahusishwa na Mashetani Wekundu



SIKU ZA LOUIS VAN GAAL ZAHESABIKA MANCHESTER UNITED NORWICH IKIFANYA KITU MBAYA OLD TRAFFORD ...Jose Mourinho ahusishwa na Mashetani Wekundu
Jerome finds the net from close range to give Norwich an            unexpected lead against Manchester United
Kibarua cha Louis van Gaal kinazidi kuning'inia pabaya baada ya Manchester United kulambwa 2-1 na Norwich katika uwanja wa Old Trafford kwenye mchezo wa Premier League.

Kipigo hicho kimeishusha United hadi nafasi ya tano, ikiipisha Tottenham iliyopanda hadi nafasi ya nne baada ya kuinyuka Southampton 2-0.

Mashabiki wa United pamoja na wachambuzi wa soka wamezidi kumuondolea uvivu Van Gaal ambapo sasa wengi wao wanamtaka kocha aliyetimuliwa Chelsea Jose Mourinho apokee kijiti Old Trafford.

Nahodha Wayne Rooney akicheza mechi yake ya 500 kwa United, akashuhudia Norwich ikipata mabao mawili ya kuongoza kupitia kwa Cameron Jerome dakika ya 38 na Alex Tettey dakika ya 54 kabla ya Anthony Martial hajafunga bao la kufutia machozi dakika ya 66.

Man Utd (4-2-3-1): De Gea 5.5; Young 6, Jones 5, Smalling 6, Blind 6; Fellaini 6 (Herrera 60 6), Carrick 5.5; Martial 6.5, Mata 6, Depay 5.5; Rooney 5

Norwich (4-5-1): Rudd 6; Martin 6.5, Bennett 6, Bassong 6, Olsson 6; Redmond 7.5, Hoolahan 6.5 (Howson 66 5.5), Tettey 6.5, O'Neill 6 (Mulumbu 81), Brady 6; Jerome 7 (Mblokani 81)
Presha kwa Louis van Gaal baada ya kucheza mchezo wa sita kwenye mashindano yote bila ushindi
Alex Tettey unleashes a                  drive to hand Norwich the lead in their clash with                  Manchester United at Old TraffordAlex Tettey akiifungia Norwich bao la pili
Cameron Jerome (wa pili kulia) anafunga goli la kwanza
Manchester United keeper                  David de Gea looks dejected after failing to keep out                  Jerome's opening goal
Kipa wa Manchester United David de Gea akiwa hoi
New signing Anthony Martial                  set up a nervous finish after pulling a goal back                  following confusion in the Norwich box
Anthony Martial akiifungia United bao pekee
Youngster Martial received                    the Golden Boy award, for the best young player in                    Europe, ahead of the gameKinda Martial akipokea tuzo ya  Golden Boy kama mchezaji bora chipukizi barani Ulaya, tuzo hiyo ilitolewa kabla ya mchezo dhidi ya Norwich haujaanza
Nahodha wa Manchester United  Wayne Rooney nae alikabidhiwa taji na Sir Bobby Charlton kwa kuucheza mchezo wa 500 kwa klabu hiyo




Comments