SERIGIO AGUERO ATAKA MANCHESTER CITY IMSAHAU LIONEL MESSI



SERIGIO AGUERO ATAKA MANCHESTER CITY IMSAHAU LIONEL MESSI
Sergio Aguero amezipuuzia ripoti zinazodai Manchester City inaweza ikamsajili Lionel Messi katika usajili wa dirisha la kiangazi.

Aguero mshambuliaji tegemeo wa Manchester City akadai kuwa Messi yuko na furaha Barcelona na itakuwa vigumu kwake kuachana na marafiki zake na Nou Camp.

City imekuwa ikihusishwa na usajali wa bei mbaya kwa supastaa huyo mwenye umri wa miaka 28, dili ambayo lingemuunganisha na nyota mwenzake wa Argentina - Sergio Aguero.

Hata hivyo Aguero amepunguza kasi ya uvumi huo kwa kuweka wazi imani yake kuwa Messi yuko katika mazingira mazuri ya kuutumikia mkataba wake unaokwenda hadi mwaka 2019.
Sergio Aguero (right) has                  played down reports suggesting Lionel Messi (left) could                  leave Barcelona Sergio Aguero (kulia) amefutilia mbali uvumi wa Lionel Messi (kushoto) kuondoka Barcelona 
Messi (right) and Aguero                  (left) know each other well having played together with                  the Argentina national team
Messi (kulia) na Aguero (kushoto) wanajuana vizuri na wamekuwa wakicheza pamoja katika timu ya taifa ya Argentina
Aguero believes Messi,                  pictured receiving his Dubai Globe soccer award, could                  play in any country
Aguero anaamini Messi, anayeonekana pichani akipokea tuzo ya  Dubai Globe soccer award, anaweza kucheza katika nchi yoyote


Comments