Spurs hawasemwi sana na ndicho wanachokifurahia kwa sasa. Naamini hata kocha wao Gregg Popovich anapenda kuona namna ambavyo Golden State Warriors wamekamata vyombo vya habari na kutawala vinywa vya mashabiki.
Lakini hii haiwafanyi San Antonio Spurs wabweteke au kukata tamaa. Wamejidhatiti sana, na ndio kwa namna moja amanyingine timu ambayo inaweza kuifunga Golden State Warriors kwa urahisi sana sana.
Alfajiri ya leo wameendeleza rekodi yao bora huku mchezaji wake Kawhi Leonard akiendelea kuiongoza timu yake vyema. Na sasa ni rasmi unaweza kuamini tu naye yupo katika mbio za kugombea tuzo ya MVP nyuma ya Stephen Curry. Anafunga wastani mzuri wa pointi na anakaba inavyotakiwa kwa kiwango kikubwa mno.
Leo aliiongoza timu yake kwa kufunga pointi 19 huku akidaka rebound 6 na timu yake ikaibuka na ushindi wa 108-83 dhidi ya Minnesota Timberwolves. Lakini hakuishia hapo ulinzi wake kwa mchezaji Andrew Wiggins kwa kiasi kikubwa uliamua mchezo huo.
Danny Green alitoka mafichoni baada ya kutokuwa na msimu mzuri wa ufungaji, na aliweza kupata pointi 11 na rebound saba. Alipata mitupo 3 kati ya 4 ya pointi 3. San Antonio sasa imeshinda mchezo wake wa 7 mfululizo huku ikiwa na rekodi ya 25-5. LaMarcus Aldridge aliongeza point 12 na rebound 8.
Karl Anthony Towns yeye aliifungia Minnesota pointi 10 na kudaka rebound 11. Zach LaVine alifunga pointi 17.
KEVIN GARNET VS TIM DUNCAN
Kevin Garnet na Tim Duncan walikutana kwa mara ya 44 katika mechi za kawaida za ligi. Jambo la kufurahisha ni kuwa takwimu zao zinashabiiiana kupita kiasi. Katika Mechi 43 zilizopita Tim Duncan alikuwa na wastani wa pointi 19.4, rebound 12.1, pasi 3.2 na blocks 1.8. Kevin Garnet yeye ana wastani wa pointi 19.1, rebound 10.4, pasi 4.1 na block 1.9.
Duncan alikuwa anapata asilimia 46 ya mitupo yake, huku Kevin Garnet maarufu kama big ticket yeye akipata asilimia 45 wote katika wastani wa dakika 37.3. Kwa ushindi wa leo Duncan ameibuka na ushindi katika michezo 27 dhdi ya 17 ya Garnet.
HIGHLIGHTS
Comments
Post a Comment