ROONEY ASEMA WANAPAMBANA KUOKOA KIBARUA CHA VAN GAAL MANCHESTER UNITED





ROONEY ASEMA WANAPAMBANA KUOKOA KIBARUA CHA VAN GAAL MANCHESTER UNITED
Wakati presha ya kupoteza kibarua ikizidi kumwandama kocha wa Manchester United Luis van Gaal, nahodha wa klabu hiyo Wayne Rooney amesisitiza kuwa wanapigana kwaajili ya kumwokoa kocha wao.

United imeshindwa kuokota ushindi katika mechi sita za mwisho za mashindao yote hiyo ikiwa ni pamoja kutupwa nje kwenye Champions League katika hatua ya makundi na kushushwa kwenye 'top four' ya Premier League.

Hatua hiyo imepelea kibarua cha Van Gaal kuwa kitanzini huku mashabiki wa United pamoja na baadhi ya wachambuzi wa soka wakimshutumu kocha huyo kwa mfumo wake wa ufundishaji.

Van Gaal mwenye umri wa miaka 69 alikatisha mapema mkutano wake na waandishi wa habari Jumatano kufuatia uvumi kuwa kocha aliyetimuliwa Chelsea Jose Mourinho yuko mbioni kurithi nafasi yake Manchester United.

Lakini pamoja na hayo, Rooney amesema bado wana imani na kocha wao na wanapambana kwaajili yake na kwaajili ya timu.

Wayne Rooney has told Sky                  Sports that Manchester United players are still fighting                  for Louis van Gaal
Wayne Rooney asema wanapambana kumwokoa Louis van Gaal
Pressure is                    mounting on the Dutchman after a winless run of six                    games and criticism over his style of play
Van Gaal yupo kwenye presha kubwa
United players                    leave the pitch after a 2-1 home defeat by Norwich,                    which saw them slip out of the top four
Wachezaji wa United wakitoka uwanjani baada ya kulambwa 2-1 na Norwich na kuenguliwa kwenye Top Four
The Dutchman                      leaves the pitch at Old Trafford with the sound of                      dissenting voices ringing in his ears
Van Gaal akiondoka Old Trafford  baada ya mchezo huku mashabiki wakimzodoa

Akiongea na Sky Sports, nahodha huyo wa United alisema: "Katika wiki chache zilizopita, matokeo hayakuwa mazuri kwetu na imekuwa ikitupa wakati mgumu kukabiliana na hali hiyo.

"Tunapaswa kuwa imara na kuwa na mshikamano ili kupata matokeo tunayoyahitaji.


"Kuna watu wanaongea mambo mengi ambayo wanaamini kuwa yatatokea, lakini sisi tunapambana kadri tuwezavyo kwaajili ya kocha wetu na kuokoa msimu wetu. Ni muhimu sote kuwa na mshikamano."




Comments