Hata anapokuwa kwenye fomu mbovu bado ni hatari, Cristiano Ronaldo alikosa penalti kipindi cha kwanza lakini bado akafunga mabao wawili yaliyoiwezesha Real Madrid kuinyuka Real Sociedad 3-1 na kumpa ahueni kocha aliyekalia kiti cha moto Rafa Benitez.
Muda mfupi kabla mchezo haujaanza, mashabiki waliojazana uwanjani walikuwa wakipiga makelele ya kumkandia kocha Benitez huku pia baadhi ya wachezaji wakionekana wazi kucheza chini ya kiwango chao ili kumkomoa.
Ilionekana kama vile Ronaldo amejiunga na kundi hilo la wachezaji baada ya kupaisha penalti yake lakini muda mfupi baadae akapata penalti nyingine na kuujaza mpira wavuni hiyo ikiwa ni dakika tatu kabla ya mapumziko.
Real Sociedad walisawazisha dakika ya 49 kupitia kwa Bruma kabla Ronaldo haijafungia Real Madrid bao la pili dakika ya 67 huku Lucas Vazquez aliyetokea benchi akihitimisha ushindi kwa goli la dakika ya 86.
Real Madrid XI: Navas, Danilo, Pepe, Nacho, Marcelo, Kroos, Modric (Casemiro 87), James (Kovacic 59), Ronaldo, Benzema (Lucas Vazquez 75), Bale
Real Sociedad XI: Rulli, Martinez, Aritz Elustondo, Inigo Martinez, Yuri, Markel, Illarramendi, Prieto, Canales (Pardo 45), Agirretxe (Bruma 18), Jonathas (Vela 68)
Cristiano Ronaldo anafunga kwa penalti
Ronaldo akikimbia kwenda kushangilia mbele ya mashabiki Bernabeu Stadium
Ronaldo (katikati) akishangilia na wachezaji wenzake wa Real Madrid Gareth Bale (kushoto), Marcelo (kulia) na Karim Benzema baada ya bao la kwanza
Ronaldo (kulia) akishangilia bao lake la penalti
Ronaldo na mbwembwe zake za ushangiliaji
Kinda hatari wa Ureno Bruma akishangilia bao pekee la Real Sociedad
Comments
Post a Comment