MSHAMBULIAJI wa timu ya Everton ya Ligi Kuu nchini Uingereza, Romelu Lukaku, amesema kwamba bado anapiga hesabu juu ya hatma yake.
Nyota huyo wa kimataifa wa Ubelgiji, akafichukua kuwa hana uhakika msimu ujao ataichezea timu gani.
Romelu Lukaku amesema anavutiwa na maisha ya Everton na anamshukuru sana kocha wake wa zamani Jose Mourinho kumruhusu aondoke Chelsea, hatua aliyoadi imefufua soka lake.
Pamoja na kuvutiwa na maisha ya Everton, Lukaku amesema zipo dalili za ofa nyingi kutoka kwa klabu kadhaa kubwa Premier League na barani Ulaya kwa ujumla.
Miongoni mwa timu anazohusishwa nazo Lukaku ni klabu yake zamani – Chelsea ambayo kwa mismu huu safu yake ya ushambuliaji imekuwa butu.
Romelu Lukaku mwenye umri wa miaka 22, amefungia Everton magoli 15 katika mashindano yote msimu huu.
Aliichezea Everton kwa mkopo kabla Mourinho hajakubali kumuuza jumla kwa klabu hiyo ya Merseyside mwaka 2013 na kutokea hapo, Lukaku amekuwa mmoja wa washambuliaji bora wa Premier League.
Romelu Lukaku akipewa nasaha na Jose Mourinho enzi hizo wote wakiwa Chelsea
Comments
Post a Comment