ROMAN ABRAMOVICH ASEMA PEP GUARDIOLA LAZIMA ATUE CHELSEA …amwandalia mshahara mnono, fungu kubwa la usajili, Guardiola asema Chelsea inahitaji wachezaji 10 wapya
Chelsea inatarajia kuwa maisha ya London yatakuwa kivutio cha wao kumnyakua kocha wa Bayern Munich Pep Guardiola mbele ya Manchester City.
Mabingwa hao watetezi wa Premier League wanaandaa ofa nono ili kuipiku Manchester City ambayo ilikuwa imekaa sehemu nzuri kupata huduma ya kocha huyo bingwa wa soka la 'draft'.
Tajiri wa Chelsea Roman Abramovich amekataa kukata tamaa ya kumnasa Guardiola - ambaye aliikwepa Chelsea mwaka 2012.
Daily Mail la Uingereza limefichua kuwa Abramovich amedhamiria kumfanya kocha huyo awe kocha anayelipwa pesa nyingi duniani kuliko kocha mwingine yeyote yule, ikiwa ni pamoja na kumpa fungu nono la kukifumua kikosi chake.
Chelsea inaamini inampeleka Pep Guardiola Stamford Bridge
Guardiola amethibitisha kuwa anaondoka Bayern mwishoni mwa msimu huu
Tajiri wa Chelsea Roman Abramovich atampa Guardiola fungu la kukifumua kikosi
Chelsea inaamini mke wa Guardiola, Cristina (kulia), anapendelea zaidi maisha ya London
Abramovich alikuwa akimlipa Jose Mourinho pauni 250,000 kwa wiki (pauni milioni 12 kwa mwaka) kabla hajaamua kumtimua Alhamisi iliyopita.
Daily Maily linaadikia pia kuwa Guardiola ameshakifanyia tathmini kikosi cha Chelsea na kusema kuwa klabu hiyo itahitaji kusajili wachezaji 10 wapya msimu ujao.
Comments
Post a Comment