Mwimbaji wa muziki                    wa injili kutoka nchini Afrika ya Kusini,Rebecca                      Malope  akiwasili kwenye uwanja wa ndege                    wa JNIA jioni hii tayari kwa ajili ya kutumbuiza kaika                    tamasha la Krismass litakalofanyika ndani ya ukumbi wa                    Diamond Jubilee jijini Dar es salaam kesho                    likishirikisha waimbaji mbalimbali wakiwemo wa nchini                    Tanzania kama vile Rose Muhando, Upendo Nkone, Joshua                    Mlelwa na wengine wengi , kushoto katika picha                    anayefurahia ni Mkurugenzi wa Kampuni ya Msama                    Promotion iliyoandaa na kumleta mwimbaji huyo  Bw.                    Alex Msama.
                  Rebecca                      Malope akiwasalimia baadhi ya mashabiki wake (hawapo                      pichani) waliokuja kumlaki mara baada ya kuwasilia uwanja                    wa ndege wa JNIA jioni hii tayari kwa ajili ya                    kutumbuiza tamasha la Krismass litakalofanyika ndani                    ya ukumbi wa Diamond Jubilee jijini Dar es salaam                    kesho 
                 Marope akikaribishwa kwa                  upendo na baadhi ya wafanyakazi wa kampuni ya Msama                  Promotions.
                 Rebecca Malope                    Mwimbaji wa muziki wa injili kutoka nchini Afrika ya                    Kusini akizungumza na mratibu wa tamasha hilo Bw.                    Hadson Kamoga mara baada ya kuwasili kwenye uwanja wa                    ndege wa JNIA jijini Dar es salaam.
                Rebecca                    Malope Mwimbaji wa muziki wa injili kutoka nchini                    Afrika ya Kusini akisisitiza jambo huku akitabasamu                    alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari wakati                    alipowasili kwenye uwanja wa ndege wa JNIA.
         Rebecca Malope                    Mwimbaji wa muziki wa injili kutoka nchini Afrika ya                    Kusini akizungumza na waandishi wa habari mara baada                    ya kuwasili nchini kwenye uwanja wa ndege wa JNIA                    jijini Dar es salaam, waliosimama nyuma Bw. Alex Msama                    na mmoja wa waratibu wa tamasha hilo Hadson Kamoga.
        





Comments
Post a Comment